TRANSLATE THIS BLOG

Wednesday, September 5, 2012

Usain Bolt kuichezea Manchester United!!

USAIN_BOLT_MAN_UNITED.png

Usain Bolt, ambae ni Mtu mwenye mbio za kasi kupita Binadamu yeyote Duniani, ataichezea Manchester United katika Mechi ya Kirafiki na Real Madrid Msimu ujao.

Mara tu baada ya kunyakua Medali za Dhahabu kwenye Michezo ya OLIMPIKI LONDON 2012, Usain Bolt alikuwa mgeni wa heshima kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Mwezi uliopita iliyochezwa Old Trafford wakati Manchester United ikiifunga Fulham Bao 3-2 na Bingwa huyo aliwataka Mashabiki wa Man United wamsisitize Sir Alex Ferguson ili amsaini yeye kama Mchezaji.

Na sasa inaelekea ndoto ya Bolt kuichezea Man United huenda ikatimia baada ya Meneja wa Man United, Sir Alex Ferguson, kudokeza kumwalika Bingwa huyo kucheza Mechi ya Kirafiki na Real Madrid.

Ferguson amesema: “Bolt ni Mtu jasiri na mpenzi mkubwa wa Man United. Inavutia akisema anataka kuichezea Klabu hii. Mwakani tunaweza kumwita acheze Mechi ya Kirafiki na Real.”

Bolt, Miaka 25, ameshawahi kufanya mazoezi na Man United.

Mechi hiyo ya Kirafiki na Real Madrid imepangwa Tarehe 3 Juni 2013 na, na kama ilivyofanywa Mwezi mmoja uliopita ilipochezwa huko Santiago Bernabeu, Mechi hiyo ambayo itachezwa Old Trafford, itawashirikisha Wachezaji Maveterani waliowahi kuchezea Klabu hizo Kongwe.


No comments:

Post a Comment