TRANSLATE THIS BLOG

Wednesday, September 5, 2012


LISTI ya FIFA UBORA DUNIANI: Spain palepale, Bongo yashuka nafasi 4 ipo 132!

>>>KUMI BORA, Ni Portugal pekee imepanda nafasi 1!!

>>>BRAZIL Wapanda 1, Wapo wa 12!!

Spain, ambao ndio Mabingwa wa Ulaya na Dunia, wameendelea kushika Nambari Wani kwenye Listi ya FIFA/Coca Cola ya Ubora Duniani iliyotolewa leo huku Tanzania ikiporomoka nafasi 4 na kushikilia Nambari 132 lakini kwenye Kumi Bora hamna mabadiliko yeyote isopokuwa Portugal kupanda nafasi moja na kushika nafasi ya 4 huku Uruguay ikishuka nafasi moja na kukamata ya 5.

Brazil, Mabingwa wa Dunia mara 5, wamepanda nafasi moja na sasa wapo nafasi ya 12.

Kwa Afrika, Timu ambayo iko juu kabisa ni Ivory Coast iliyobaki nafasi yake ile ile ya 16.

Listi nyingine mpya itatolewa Oktoba 3.

KUMI BORA:

[Kwenye Mabano nafasi za Mwezi uliopita]

1. (1) Spain

2. (2) Germany

3. (3) England

4. (5) Portugal

5. (4) Uruguay

6. (6) Italy

7. (7) Argentina

8. (8) Netherlands

9. (9) Croatia

10. (10) Denmark

No comments:

Post a Comment