TRANSLATE THIS BLOG

Monday, September 10, 2012


Raheem Sterling, Livermore na Lallana wachukuliwa England!!

RAHEEM_STERLING.png

Kocha wa England Roy Hodgson amelazimika kumchukua  kinda wa Liverpool Raheem Sterling, Chipukizi wa Tottenham Hotspur Jake Livermore na yule wa Southampton Adam Lallana ili kuongeza nguvu Kikosi chake kwa ajili ya Mechi ya Kundi H ya Kombe la Dunia dhidi ya Ukraine itakayochezwa Jumanne Usiku Uwanjani Wembley baada ya Kikosi chake kukumbwa na upungufu kufuatia Theo Walcott kuondoka baada ya kuugua.

Mbali ya Walcott, Straika wa Chelsea, Daniel Sturridge, nae anaugua na huenda asiwepo hiyo Jumanne.

Walcott amekuwa Mchezaji wa 5 kuondoka kwenye Kikosi cha sasa cha England na wengine ni majeruhi John Terry, Ashley Cole, Adam Johnson na Andy Carroll na kuifanya Timu ibakiwe na Wachezaji 18 tu.

Upungufu huu, hasa kuondoka kwa Walcott na kuugua kwa Sturridge, kumemfanya Kocha Hodgson aite Chipukizi kuimarisha Kikosi.

Uteuzi wa kushangaza wa Hodgson ni kumwita Winga Raheem Sterling wa Liverpool [Pichani], mwenye Miaka 17 tu, ambae ameichezea Liverpool Mechi 5 tu.

Hata hivyo Sterling, Mzaliwa wa Jamaica, amewahi kuchezea Timu za Vijana za England za U-17 na U-19.

Jake Livermore wa Tottenham, mwenye Miaka 22, amewahi kuichezea England Mechi moja alipotokea benchi na kucheza na Italy kwenye Mechi ya Kirafiki Mwezi uliopita.

Winga Lallana, Miaka 24, amewahi kuichezea mara moja tu Timu ya Vijana ya England ya U-21 na hii ni mara ya kwanza kuitwa kwenye Kikosi cha Kwanza.

Akiongelea uteuzi wake huu, Hodgson amesema: “Hii ni nafasi nzuri kuwaita Wachezaji Vijana waje kuona mambo. Bado tunao Wachezaji wa kutosha kukabili upungufu kwa Mechi na Ukraine lakini vyema pia ukawa na hawa Vijana!”

Pengine tatizo kubwa kwa Hodgson ni kuamua nani atachukua nafasi ya John Terry kwenye Sentahafu kati ya Gary Cahill na Phil Jagielka.

No comments:

Post a Comment