TRANSLATE THIS BLOG

Thursday, September 6, 2012


Arshavin aikataa Dinamo Moscow

Andrey Arshavin alikataa kujiunga na klabu ya Russia,Dinamo Moscow,siku ya mwisho ya dirisha la usajili kufungwa na kutaka kuendelea  kusalia Emirates kupigania namba katika kikosi cha kwanza.

 

Arsenal walimpa  Arshavin, 31,offer ya kujiunga kwa mkopo wa mwaka mmoja na  Dinamo lakini tofauti na matarajio mrusi huyo alikataa.

Meneja wa Dinamo, Dan Petrescu amethibitisha  maamuzi ya Arshavin: na kusema kuwa nilikuwa namuhitaji mchezaji huyo lakini Andrey akasema hapana kwa  Dinamo."

Nahodha hhuyo wa Russia alipoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza Arsenal msimu uliopita  na kucheza kwa mkopo katika klabu yake ya zamani ya Zenit St Petersburg.

Arsharvin katika msimu wote alikuwa akihusishwa na vilabu vya Russia ,Zenit na  CSKA Moscow  ambazo zilionyesha nia yakumuhitaji moja kwa moja…

Siku zilizopita , Arshavin alisema angependelea kurudi nyumbani na kuichezea klabu yake aipendayo ya  Zenit.

No comments:

Post a Comment